Description
Viungo: Cassia Seed, Fructus Lycii, White Chrysanthemum, Root of Dahurian Angelica, Rhizoma Dioscoreae, Dandelion
Kazi na Faida za livergen;
- Kuchochea utoaji sumu mwilini
- Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mishipa midogo ya ini na kuimaarisha utendaji wa ini
- Kusaidia ujenzi wa seli mpya za ini
- Kupunguza kasi ya kuharibika kwa ini (liver cirrhosis) kunakochangiwa na ini kuwa na mafuta, hepatitis na utumiaji wa pombe
- Kuzuia uharibifu wa ini kutokana na kemikali, metali nzito, madawa, sumu ndani ya chakula na vichafuzi vingine.
Inafaa Kutumika Kwa:
- Watu wanaotaka kuondoa sumu katika miili yao
- Watu wenye matatizo ya ini kama mafuta (Fatty liver), homa ya nyongo ya manjano (jaundice), liver cirrhoses na magonjwa mengine
- Watu wenye magonjwa ya nyongo (cholecytitis), kokoto ndani ya nyongo (gallstone), wenye homa ya nyongo ya manjano au wenye matatizo mengine ya nyongo
- Watu wanotumia sana pombe
Watu wanaoishi kwenye mazingira hatarishi
Maelezo Muhimu:
Ini ni kiungo kikubwa kinachopatikana upande wa kulia wa tumbo. Ini linajulikana kufanya kazi zaidi ya 500 na kwa sababu hiyo huitwa maabara ya mwili wa binadamu. Ini linahusishwa na utendaji kazi wa viungo vyote vya mwili kwa sababu hufanya kazi ya kuchuja chakula na majimaji yote yanayoingia. Mwili hulitegemea ini katika kuondoa sumu na kwa sababu hiyo linahusishwa na magonjwa yote au matatizo yote yanayotokea katika mwili wa binadamu. Zifuatazo ni kazi za ini
- Kujenga na kuvunja protini, mafuta, na wanga, na hivyo kutoa nishati na virutubisho
- Kutunza vitamini, madini na sukari
- Kuchuja damu na kusaidia kuondoa kemikali mbaya na bakteria wabaya
- Huzalisha nyongo inayochakata mafuta
- Hutunza damu ambayo inaweza ikatolewa mara itakapohitajika
- Hutengeneza protini za maji (serum proteins) ambazo hulinda uwiano wa maji mwilini na kutumika katika usafirishaji.
- Husaidia kulinda kiwango cha maji na electrolyte.
- Huzalisha chembechembe za kinga kama gamma globulin
- Huvunja na kuondoa homoni za ziada
- Huzalisha urea, hujenga protini ya damu, na kuzibadilisha amino acids
- Huondoa chembechembe nyekundu za damu zilizoharibika.Hii ni sehemu tu ya orodha ndefu ya kazi za ini. Haijajulikana kiuhakika ni shughuli ngapi za mwili zinasimamiwa na ini.Magonjwa Ya Ini:
Vitu vingi vinaweza kusababisha magonjwa ya ini. Hivi ni pamoaja na maambukizi ya hepatitis B, chakula kisichojitosheleza, uchafuzi wa hewa, uvutaji wa sigara, uchovu wa muda mrefu, mafua makali, na kadhalika.Livergen Capsule Inasaidiaje?
Livergen Capsule inayotengenezwa na Green World inaboresha mzunguko wa damu katika ini na pia katika mishipa midogo iliyo ndani ya ini; inasaidia ukarabati wa seli za ini zilizoathirika. Hurudisha utendaji kazi wa ini lililoshambuliwa na kuwa wa kawaida na kuboresha shughuli za utoaji sumu za ini. Hizi ni sababu tosha kukufanya ununue livergen.
Reviews
There are no reviews yet.