Description
Viungo ndani ya chai ya basalm:
Balsam Pear Powder, Green Tea Powder
Kazi na Faida za chai ya Basalm
- Kuimarisha Beta cells za kongosho linalohusika na utoaji wa kichocheo insulin,
- Kuzuia ufyonzwaji wa sukari katika utumbo mdogo, na hivo kupunguza sukari kwenye mzunguko wa damu
- Kuepusha madhara ya kisukari kama kiu na kukauka mate.
Yafaa zaidi kutumiwa na
- Watu wenye upungufu wa sukari katika damu
- Watu wenye ugonjwa wa kisukari
Ufanyaji Kazi wa Balsam Pear Tea:
Balsam Pear ambayo pia hujulikana kwa majina ya “cool melon” au “bitter gourd”, ina viwango vikubwa vya vitamini B1, vitamini C na madini. Huondoa kiu, huuburudisha mwili na kuongeza kasi ya ufanyaji kazi ya mwili. Husaidia mmeng’enyo wa chakula na kuondoa tatizo la kutopata choo.
Balsam pear iligundulika pia kuwa kiambata cha lectin yenye tabia za insulin na kwa sababu hiyo huitwa insulin ya mimea (plant insulin). Uwepo wa lectin una faida ya kuzuia kupata kisukari katika umri mkubwa, au kisukari kinachoitwa Type II diabetes.
Ukinywa balsam pear tea, kwanza utasikia uchungu halafu utamu kwa mbali. Unywaji wa balsam mfululizo hauzuii kisukari peke yake bali hukuongezea mwilini vitamini mbalimbali na madini.
Kiungo muhimu ni insulin itokanayo na mimea – plant insulin – ambacho huboresha ufanyaji kazi wa kongosho, kuamsha seli za Beta (B-cells), kuondoa madhara ya kisukari, kurekebisha lipids kwenye damu, kupunguza pressure ya damu, kuamsha seli za kongosho na kuongeza kasi ya oksijeni kuifikia glucose.
Madhara Ya Kisukari
- Kuharibu mishipa mikubwa ya damu: Magonjwa ya kiharusi, uharibu wa moyo kutokana na ukosefu wa damu kwenye misuli ya moyo (myocardial infarction), kufa kwa seli na kuoza (gangrene) kwa viungo vya mwili vilivyo sehemu ya chini ya mwili.
- Kuharibu vijishipa vidogo vya damu: Kwenye macho husababisha uharibifu wa lensi ya macho (cataract), uharibifu wa neva (optic nerve) na kusababisha kutoona vizuri au upofu, na matatizo mengine ya macho.
- Kuharibu mfumo wa fahamu.
- Kukatwa viungo vya mwili.
Reviews
There are no reviews yet.