Description
Viungo: B-Carotene na Lycopene
Kazi Na Faida Za Kirutubisho cha Lycopene
- Huurutubisha mwili na vitamini A
- Hufanya kazi kama antioxidant yenye nguvu na kuondoa radikali huru
- Huzuia kansa na hasa kansa ya tezi dume
- Huzuia atherosclerosis kwa kupunguza lipids kwenye damu
Yafaa Kutumiwa Na
- Watoto na watu wazima wenye upungufu wa vitamini A
- Wanaume wenye matatizo ya tezi dume kama prostatitis, tezi iliyovimba (BPH), na kansa ya tezi dume
- Watu wenye cholesterol kwa wingi
Maelezo Muhimu kuhusu B-crotene na Lycopene
Ufanyaji Kazi Wa B-Carotene Kama Vitamini A
B-carotene ni rangi ya asili (nyekundu-rangi ya chungwa) na nadni ya karoti inayozifanya kuwa na rangi ya chungwa na ndiyo namna carotene inavyokuwa katika mimea. Molekuli moja ya B-carotene huweza kuvunjwa na vimeng’enya vilivyoko ndani ya utumbo na kupata molekuli mbili za vitamini A, ambayo huchochea kujigawa kwa seli, husaidia mwili kukua, na huongeza kasi ya kujikarabati kwa seli za tishu zinazofunika viungo vya ndani ya mwili (epithelial tissue) na ukuaji wa sebum. Ni muhimu kwa ukuaji wa mifupa, meno, watoto na kulinda uwezo wa kuona.
B-Carotene & Lycopene Kama Antioxidant
Kwa kuwa ni mchanganyiko muhimu wa flavonoid, B-Carotene ina tabia za nguvu za antioxidant, inasaidia kupambana na radikali huru(free radicals) na hivyo kupunguza madhara yake kwenye utando unaofunika seli, DNA na protini kwenye seli. Lycopene ni carotene ang’avu nyekundu inayopatikana ndani ya nyanya na ndani ya matunda na mboga nyingine nyekundu. Umbo la lycopene linairuhusu kushambulia radikali huru ambazo ni sumu mwilini kirahisi kutoka maeneo yanayoizunguka, na kuifanya kuwa antioxidant ya nguvu.
B-Carotene & Lycopene katika kuzuia na kupambana na saratani
B-Carotene huzuia carcinogen zisishambulie DNA kwenye kiini cha seli. Huzuia kusambaa kwa seli za kansa hivyo kuzuia kansa kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ripoti ya kisayansi iliyoandaliwa na mabingwa wa tiba wa Marekani mwaka 1989 inaonyesha kuwa lycopene huzuia ukuaji wa saratani ya tezi dume.
B-Carotene & Lycopene katika kusafisha damu
Lipids zilizomo ndani ya damu mara nyingi ni triglyceride, cholesterol, phospholipids. Nyingi ya hizi huungana na protini na kujenga lipoprotein ambayo huganywa katika makundi mawili, low density lipoprotein (LDL) na high density lipoprotein (HDL).
Ikiwa kiwango cha LDL au cholesterol mbaya katika damu kitakuwa kikubwa, kipenyo cha arteri kitakuwa kidogo, atherosclerosis hutokea na uwezekano wa kupata mshituko wa moyo (heart attack) huwa mkubwa. Hii ndiyo sababu LDL huitwa “bad cholesterol”.
Kiwango kikubwa cha HDL(cholesterol nzuri) hulinda dhidi ya magonjwa ya moyo kwa kutoa LDL nje ya mfumo wa damu. Hii ndiyo sababu HDL huitwa “good cholesterol”. B-Carotene na lycopene vyote huwasaidia watu wenye umri mkubwa kuzuia kuganda kwa damu na kupunguza uwezekano wa kupata mshituko wa moyo.
Reviews
There are no reviews yet.